Charles Kimei 'bye bye' CRDB......soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei
ametangaza kuwa hataongeza mkataba wake mara utakapofikia ukomo Mei 31, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari, amesema amekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha
miaka 20 hivyo umekaribia wakati wake wa kumwachia mtu mwingine.
“Nimekuwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB kwa takribani
miaka 20 sasa, hivyo wakati umekaribia kwangu mimi kumwachia mtu mwingine
nafasi hii na mimi kuendelea kufanya majukumu mengine,” amesema Dk. Kimei.
Ameongeza “Kufuatia sera ya kurithisha nafasi ya mkurugenzi
mtendaji wa Benki yetu hii, ifikapo Januari 2018, Bodi ya Benki inalazimika
kuanza mchakato kwa ajili ya kujaza nafasi hii muhimu kwa mustakabali wa Benki
ya CRDB,”
Dk. Kimei amesema mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mtendaji mpya umekwisha anza na sababu ya kuanza mapema ni ili kuhakikisha zoezi
linafanyika kwa uangalifu na kutoa muda wa kutosha wa kupata uidhinisho wa
mamlaka husika kwa mtu atakayechaguliwa kushika nafasi hiyo.
Amewahakikishia wateja wa benki hiyo na watanzania kwamba
benki ni salama na itaendelea kuwa salama.
“Tunatangaza hili mapema ili kuepusha dhana au hisia ya
kwamba mkurugenzi mkuu anaondoka kwa vile kuna tatizo, au benki inaweza
kuyumba. Niko kwa takribani miezi 18 na mioyo ya wateja ibaki na amani,”
amesema.
No comments:
Post a Comment