Yanga, Simba, Azam kutua Zanzibar Januari mosi....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza rasmi kesho ambapo jumla ya michezo mitatu itachezwa huku Simba, Yanga na Azam zikitarajiwa kuwasili Januari Mosi, 2018.
Kikosi cha timu ya soka ya YangaMichuano hiyo ambayo itachezwa katika uwanja wa Aman mjini Unguja, itachezwa kuanzia majira ya saa 8:00 mchana na ufunguzi rasmi utakuwa majira ya saa 10:00 za jioni.
Katibu msaidizi kamati ya kusimamia mashindano hayo Khamis Shaali amesema saa 8:00 kutakuwa na mchezo kati ya Mlandege na JKU, saa 10:00 Jamhuri itapambana na Mwenge huku majira ya saa 2:00 usiku kutakuwa na mchezo utakaowakutanisha Zimamoto na Taifa ya Jang’ombe.
Amesema maandalizi ya michuano hiyo imekamilika na timu ya Mwenge kutoka Pemba iliwasili jana na Jamhuri inawasili leo.
Amesema timu kutoka Pemba zinajitegemea huku timu kutoka Tanzania Bara ambazo ni Yanga, Azam, Singida United na Simba zitapangiwa Hoteli.
“Tumeenda kuweka 'booking' katika hoteli mbili moja ni Zanzibar Ocean View na nyingine ni Maruhubi Beach Villa lakini bado hatujalipa fedha za mwanzo kwa hiyo hatujajua ni ipi kati ya hiyo tutaziweka timu hizo,” amesema.
Jumla ya timu 11zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambapo kwa Zanzibar timu zinazoshiriki ni JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Mlandege, Jamhuri na Mwenge na kwa Tanzania Bara ni Simba, Yanga, Azam FC na Singida United na kwa nje ya Tanzania ni URA ya Uganda
No comments:
Post a Comment