Dk Mndolwa mwenyekiti mpya jumuiya ya wazazi CCM...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Dodoma
MKUTANO mkuu wa jumuiya ya
wazazi wa CCM, leo wamemchagua Dk Edmund
Bernad Mndolwa kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya wazazi CCM, Dk. Edmund Mndolwa
Dk Mndolwa ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa, wilaya ya Korogwe vijijini mkoani Tanga, amepata kura 554,
makamu wake ni Haidar Haji Abdalah aliyepata
kura 462.
Wajumbe wa NEC kutoka
Tanzania bara ni Edward Sokoine amepata 607,
Mohammed Nasoro Ngongite amepata kura384, Paul Herman Kirigini amepata 343.
Wajumbe wa NEC kutoka Zanzibar ni Amina Ali Mohammed amepata kura 498, Juma
seleman Kimei amepata 451, wajumbe wa baraza wa jumuiya hiyo kutoka bara ni Lulu Mabasi Mtemvu ,Stephen Maji Marefu na
Sufi kasim Sudi.
Baraza kutoka Zanzibar ni Ali issa Ali, Christina Joram Anthony, Habiba
Ali Mohamedi.
Mwakilishi umoja wa wanawake
ni Bainaga Kassian Nuru na wa Uvccm ni
Omary Ajili Kalolo
No comments:
Post a Comment