NEC yaituliza Ukawa....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es
Salaam
TUME ya taifa ya
uchaguzi(NEC) imewataka wadau na vyama vya siasa kufuata utaratibu wa kisheria
na kwamba ratiba ya uchaguzi wa marudio wa ubunge na udiwani wa Januari 13,
2018 haitobadilika.
Mkurugenzi wa uchaguzi Nec,Ramadhani Kailima
Msimamo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa
uchaguzi NEC, Kailima Ramadhani alipokuwa akizungumza na matukio360.
‘’Nec inafanya shughuli zake
kwa kuzingatia na kufuata sheria hivyo wadau na vyama vya siasa ni lazima navyo
vifuate sheria katika kufanya maamuzi,’’ amesema Kailima
Amesema uamuzi wa vyama vinavyounda
Ukawa kutaka uchaguzi uahirishwe haitowezekana na zaidi wafuate taratibu za
kisheria ili kufanikisha hilo.
Jana mwenyekiti taifa wa Chadema, Freeman
Mbowe kwa niaba ya Ukawa alitaka uchaguzi uahirishwe akida mazingira hayako
sawa na kwamba serikali na Nec ikikata kufanya hivyo, vyama vinavyounda umoja
huo havitoshiriki uchaguzi huo wa ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini,
Songea mjini na Longido Kaskazini. Pia kata sita zinatarajiwa
kufanya uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment