Droo kamili ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hii hapa...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
VIONGOZI wa Ligi ya Premia,
Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United wakutana na
Sevilla wanaocheza La Liga nao Liverpool watakutana na FC Porto ya Ureno.
Chelsea wamepangwa kukutana
na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao
wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa.
Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Paris
St-Germain.
Klabu tano kutoka England zilifuzu kwa hatua ya
makundi msimu huu, ambayo ni rekodi.
Chelsea ndio pekee wa Uingereza waliofuzu wakiwa wa
pili kutoka kundi lao, klabu nyingine zote zilimaliza kileleni.
Washindi wa makundi watakuwa ugenini mechi za kwanza
13/14 na 20/21 Februari na nyumbani mechi za marudiano mnamo 6/7 na 13/14
Machi. Fainali itachezewa Kiev mnamo 26 Mei.
Droo kamili: Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya
Juventus v Tottenham
FC Basel v Manchester City
Porto v Liverpool
Sevilla v Manchester United
Real Madrid v PSG
Shakhtar Donetsk v Roma
Chelsea v Barcelona
Bayern Munich v Beskitas
No comments:
Post a Comment