Serikali yapoteza bilioni 300...soma habari kamili na matukio360..#share
Na
Salha Mohamed, Dar es salaam
MWAKA 2016 Serikali imepoteza bilioni 300 kutokana na biashara za
masoko ya bima ya nje ya nchi.
Kamishna Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za Bima (TIRA) Dk Baghayo Saqware (wapili kulia) akizungumzia uzinduzi wa waraka na:055/2017
Mkurugenzi wa Leseni na Mwenendo wa Masoko, Mamlaka ya Usimamizi
wa Shughuli za Bima (TIRA), Samwel Mwiru ameyasema hayo wakati wa uzinduzi
wa waraka na:055/2017 wa masharti ya kufanya biashara na makampuni ya bima
mtawanyo na madalali wa bima mtawanyo kutoka nje ya nchi.
Amesema katika nchi za SADC kiwango cha biashara ya nje asilimia 57 ya biashara ya bima inabaki ndani ya nchi .
"Tunapungua kwa asilimia 8,mwaka 2016 fedha ambazo
zilikwenda nje ya nchi ni bilioni 300,"amesema.
Amesema kwa waraka huo unaoweka masharti ya kufanya biashara na
makampuni ya bima mtawanyo na madalali wa bima mtawanyo kutoka nje ya nchi
utaongeza kiwango cha biashara ndani ya nchi.
Kwa upande wake Kamishna wa Bima (TIRA) Dk. Baghayo Saqware
amesema makampuni yatakayoshindwa kufuata waraka huo hawatasita kufungia leseni
zao za biashara.
Amefafanua kuwa mamlaka ilibaini matumizi hasi ya utaratibu wa
kupeleka nje biashara za bima mtawanyo kwa baadhi ya makampuni ya bima
nchini.
Amesema kuzunduliwa kwa waraka huo ni jitihada za mamlaka katika
kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kutokana na kupeleka biashara za bima
nje ya nchi kupitia utaratibu wa bima mtawanyo 'reinsurance'.
"Mamlaka ilibaini baadhi ya makampuni ya bima nchini
kufanya biashara za bima na makampuni ya bima mtawanyo yasiyo na viwango bora," amesema.
Amesema kutokana na mapungufu hayo, mamlaka imetoa waraka huo kudhibiti mwenendo hasi na kuimarisha ufanisi katika upelekaji wa biashara za
bima mtawanyo nje ya soko la bima Tanzania.
Amesema wamejidhatiti majukumu chini ya serikali ya awamu
ya tano ya John Magufuli katika dhamira ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kutoa
huduma za bima kwa wananchi na makampuni.
"Itatengeneza fursa za ajira kwa watanzania na kuongeza
mchango wa sekta ya bima katika pato la taifa, "amesema.
Waraka huo utaanza kutumika Januari mosi, 2018.
No comments:
Post a Comment