Sekretarieti maadili ya umma yatoa siku tatu kwa viongozi.....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetoa siku tatu
kwa viongozi wa umma ambao hawajatoa tamko la mali zao kufanya hivyo na watakaoshindwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Wapili kutoka kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Pia imewataka viongozi wa umma wastaafu kujaza fomu za tamko
la rasilimali na madeni na kuziwakilisha kwa kamishna ili kujua kama mali
walizonazo kwa sasa walizipata kwa halali ama la.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa
Maadili wa Sekretarieti Jaji Mstaafu Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa
habari, amewataka katika matamko hayo kuambatanisha na mali za wenza wao na
watoto wao umri usiozidi miaka 18.
“Kwa kuzingatia sheria ya maadili ya viongozi wa umma,
kifungu cha 9 (1) (b) kinamtaka kiongozi wa umma, kila mwisho wa mwaka kupeleka
kwa kamishna wa maadili tamko la maandishi katika hati rasmi linaloorodhesha
mali au rasilimali zake na za mwenza wake na za watoto wake wenye umri usiozidi
miaka 18 na ambao hawajaoa au kuolewa, mwisho wa kuwasilisha fomu hizo ni Disemba 30,” amesema Jaji Nsekela.
Jaji Nsekela amesema ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 (c)
cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kiongozi kushindwa kutoa tamko
bila sababu ya msingi.
Naye Ofisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Filotheus Manula
akitaja hatua ambazo zinawezakuchukuliwa kwa viongozi watakaoshindwa kutekeleza
matakwa ya sheria hiyo, amesema ni pamoja na kushushwa cheo.
Nyingine ni kusimamishwa kazi, kufukuzwa kazi, mwenye mamlaka
ya uteuzi anaweza kuchukua hatua stahiki na onyo kwa viongozi ambao hawana
uelewa wa kutosha juu ya sheria hiyo kutokana na kutokuwa na uzoefu huo.
No comments:
Post a Comment