Mwenyekiti CCM akamatwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Singida

JESHI la polisi mkoani Singida linamshikiria  mwenyekiti wa CCM  mkoa wa Singida Juma Kilimba kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mwanae Fatma, aliyekufa kutokana na ajali ya gari.

Desemba 25, 2017 mwenyekiti huyo, mkewe na watoto wao watatu walijeruhiwa baada ya gari alilokuwa akiendesha kupinduka eneo la Msigiri wilayani Iramba mkoani Singida.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Singida, Juma Kilimba

Kamanda wa polisi mkoani Singida amesema upelelezi wa awali unaonyesha ajali ilitokana na ubovu wa gari na kwamba 'steering road' ya gari hilo ilichomoka.

"Tunamshikiria mwenyekiti huyu wa CCM, uchunguzi wa awali unaonyesha ajali ilisababishwa na ubovu wa gari alilokuwa akiendesha hasa 'steering road' ilichomoka na kusababisha ajali na baadae kupelekea kifo cha mtoto wake Fatma," amesema

Jumatatu ya Desemba 25, 2017 Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jamson Mhagama alisema ajali hiyo ilitokea mchana  na Kilimba alilazwa katika Hospitali ya Kiomboi huku mkewe Kilimba na wanawe walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Itigi na kwamba CCM mkoani Singida inaendelea kusimamia matibabu yao.

 Pia  alisema mmoja kati ya watoto hao alikuwa akipatiwa huduma katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search