Jiji la Dar es Salaam lapokea tuzo ya kimataifa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Christina Mwagala

 KUPITIA  mradi wa mabasi yaendayo haraka, jiji  la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 Duniani  yaliyopata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .

Katika tuzo hiyo mwaka 2017 imepokelewa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8, 2017.

Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo  na Jiji la New York  la nchini Marekani.

Mradi wa mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya mafanikio ya tuzo  hiyo.

Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90 duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi Duniani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search