Kesi kigogo TRA anayemiliki gari 19, kuunguruma Januari...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
AFISA msaidizi wa forodha wa TRA, Jennifer Mushi
anayekabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki gari 19, mali isiyolingana na kipato chake halali
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu atasomewa maelezo ya awali, Januari
11,2018.
Jennifer ameshtakiwa mahakamani hapo, chini ya kifungu
cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11ya
mwaka 2007.
Leo alipaswa kusomewa maelezo hayo ya awali lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter
ameeleza mahakamani kuwa bado
hawajamaliza kuiandaa. Hivyo aliomba ipangiwe tarehe nyingine.
Hakimu Shaidi ameiahirisha
kesi hiyo hadi Januari 11,2018 ambapo mshtakiwa huyo atasomewa maelezo hayo ya
awali (PH) na kesi kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka.
Mshtakiwa huyo anadaiwa
kuwa kati ya Machi 21,2016 na Juni
30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa
mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19.
Nagari hayo ni Toyota RAV4, Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck,
Toyota Viz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota
Wish na Toyota Mark X.
Mengine ni Toyota Regiusage,
Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na
Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 Mali ambayo hailingani na
kipato chake halali.
Anadaiwa kuwa, kati ya
Machi 21 ,2012 na Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa
TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha
ambayo hailingani na Kipato chake halali.
Baada ya kusomewa mashtaka
hayo mshtakiwa huyo alikana na yupo nje kwa dhamana.




No comments:
Post a Comment