Makalla awapa mtihani watendaji Mbeya...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu
IFIKAPO mwaka 2020 wakuu wa wilaya, wakurugenzi  wa halmashauri na waganga wakuu mkoani Mbeya wameagizwa kutekeleza sera ya afya ya jamii kwa kuhakikisha kila kijiji  kinakuwa  na kituo cha afya na zahanati.

Vijiji 233 kati ya vijiji 553 vilivyo katika mpango wa kuwa na vituo vya afya,  ndio vyenye uhakika  hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 43.7

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla(katikati) akipokea  mifuko 40 ya saruji yenye thamani ya milioni 5  kutoka kwa wafanyakazi wa benki ya Akiba Commerce  kwa ajili ya ukarabati wa njia ya wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya.


Agizo hilo limetolewa leo na mkuu wa mkoa huo  Mkoa Amos Makalla  kwenye kikao cha afya cha  mkoa kilichohusisha wadau wote wa afya kilicholenga kujadili changamoto  na mafanikio  hususan mikakati ya  ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika kila kijiji.

"Hicho ni kipimo cha utendaji wa kazi ni lazima mpambane kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati na kituo cha afya," amesema Makalla.

Amesema nchi yoyote haiwezi kupiga hatua za kimaendeleo kama wananchi wake wanakosa huduma za msingi ikiwamo ya afya na kwamba wananchi washirikishwe  kuchangia miradi ya maendeleo.

Kaimu mganga mkuu wa hosptali ya mkoa, Dk Yahya Msuya amesema baada ya majadiliano ya kina na wadau wa sekta ya afya wataanza ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika kila kijiji.

Katika kukabiliana na hali hiyo pia kuna changamoto ya ukosefu
wa matumizi ya vyoo bora na ni  asilimia  68 tu wakazi ndio wanatumia vyoo bora.



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search