Kufungwa Man U Mourinho arushiwa vinywaji, alalamika...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
MKUFUNZI wa Manchester United Jose Mourinho amerushiwa
maji na maziwa kufuatia kushindwa na Manchester City huko Old Trafford jana.
Kocha Man U, Jose Mourihno
Hata hivyo Mourihno amelalamika timu yake kunyimwa
penati kipindi cha pili kunako dakika ya 20 kabla ya mechi kumalizika na
kwamba Man u walistahili kupata penati
na si kwa mchezaji wake Ander Herrera kupewa
kadi kwa kujiangusha kutokana na kuchezewa rafu na mchezaji wa Man City,
Otamendi
“Ilikuwa ni penati ya wazi naamini tungetoka suruhu ya
kufungana goli 2-2,’’ amesema Mourihno
Mashabiki Man United
walikasirika kutokana na kile walichokiona kuwa kusherehekea kupindukia kwa
City kufuati ushindi wa Jumapili wa bao 2-1 ambalo lilifungua mwaka wa pointi
11 kileleni.
Wachezaji wa City
walisherehekea na mashabiki wao baada ya kipenga cha mwisho na maafisa wengine
wakajaribu kumshawishi meneja Pep Guardiola kujiunga nao lakini akakataa.
Baada ya wachezaji kuondoka
uwanjani inaeleweka kuwa Mourinho alilalamika akiwa ndani ya chumba cha
kubadilishia nguo kabla ya kurudi kwa mahojiano.
Upande wa City ulijibu huku
kipa wa Brazil Ederson akijibizana na Mourinho kwa lugha ya kireno.
Goli la David Silva na Nicolas
Otamendi jana yalizidi kuipa uongozi wa ligi Man City na kufikisha idadi ya
mechi 40 bila kufungwa
No comments:
Post a Comment