Meya Mwita kuunguruma Addis Ababa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Christina Mwagala, Dar es Salaam
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita anatarajia kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa kujadili changamoto zinazowakabili viongozi wa serikali za mitaa.


Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita

Ameondoka Jijini Dar es salaam  jana jioni kuelekea jijini Addis Ababa, Ethiopia kunakofanyika mkutano huo.

Katika mkutano huo wa siku tatu uliondaliwa na Umoja wa Mataifa(UN) unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwamo mameya wote.

Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo  ni  suala la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka nchi mbalimbali.

Meya Mwita atazungumzia changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam  na  namna ambavyo  wameweza kuzitatua.

Pia ataelezea mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za maendeleo.


"Pamoja na mambo mengine   mkutano huu utatujengea uwezo wa kiutendaji katika shughuli zetu za kila siku," amesema Mwita.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search