Magufuli apeleka fomu zake sekretarieti ya maadili...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

RAIS John Magufuli leo amewasilisha  fomu zake za tamko la rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma katika ofisi ya sekretariati  ya maadili ya umma jijini Dar es salaam.

Hatua yake hiyo inafuatia jana sekretarieti hiyo kutoa siku tatu hadi Desemba 30, 2017 kwa viongozi wa umma kukamilisha zoezi hilo na kwamba watakaoshindwa watachukuliwa hatua za kisheria






Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akimsikiliza Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa Viongozi wa Umma Katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.(Bofya blog kwa habarin na picha)






About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search