Wakuu wa wilaya,wakurugenzi Mbeya wabanwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Mbeya

WAKUU wa wilaya , Wakurugenzi wa halmashauri  zote  mkoani hapa
wameagizwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuanza
mara moja  ukaguzi wa  maroli  ya mizigo ili kubaini njia zinazotumika
kusafirishia chakula,dawa na vipodozi vyenye viambata vya sumu kinyemela  kupitia
mpaka wa Malawi na Zambia.
Wakuu wa wilaya,wakurugenzi mkoani Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla hayupo pichani hii leo

Pia wakurugenzi wameagizwa  kufanya operesheni ya kukagua bidhaa
zinazoingizwa katika masoko yote hususan  maduka  ya vipodozi  ,
bucha za nyama,  samaki na machinjio ya mifugo  ili kubaini ubora wa
vyakula vinavyoingizwa kwa lengo la kulinda afya za watumiaji.

Mkuu wa   Mkoa Amos Makalla, ametoa maagizo hayo leo , kwenye kikao
cha kujadili sheria za chakula , dawa na vipodozi kilichohusisha Wakuu
wa wilaya, Wakurugenzi ,Waganga  wakuu wa wilaya, Wakuu wa Idara,
Maofisa afya na kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa jijini
hapa.
Amesema  jukumu  la kufanya ukaguzi  sio la TFDA pekee bali
linawahusu wote kutokana na  halmshauri kukasimishwa majukumu  katika
maeneo yao kufanya ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa na kutoka nchi
hususan dawa,chakula na vipodozi.


"Nimebaini halmashauri hamtekelezi majukumu mliokasimishwa na TFDA
sasa ninaagiza kuanzia sasa  mkaanze utekelezaji wa agizo langu
hususan katika mipaka ya nchi jirani ya Zambia na Malawi kwani kuna
zaidi ya njia za kipanya 300 zinazotumiwa na wafanyabishara kuingiza
bidhaa nchini "amesema.


Meneja wa  (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Rodney  Alananga
amesema ushirikiano mzuri baina  wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa
halmashauri  mkoani hapa, utaleta tija katika kutokomeza uingizwaji wa
bidhaa  kiholela.


Mkaguzi wa TFDA, Kanda ,  Poul Sonda alisema kufuatia changamoto ya
baadhi ya wafanyabishjara kuuza bidhaa zisizo na ubora elimu imekuwa
ikitolewa mara kwa mara na lengo  ni kusaidia jamii iwe na afya bora
katika kuelekea uchumi wa viwanda.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search