Mambosasa awataka polisi kuwa 'nga'ng'ari'...soma habari kamili na matukio360..# share
Na mwandishi wetu
KAMANDA wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewasisitiza askari kufanya mazoezi ya viungo.
KAMANDA wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewasisitiza askari kufanya mazoezi ya viungo.
Askari polisi kanda maalum ya Dar es Salaam wakifanya mazoezi.
Amesema hayo leo
aliposhiriki katika matembezi na mazoezi ya viungo na askari wa vikosi vya
kanda maalum ya Dar es Salaam.
“Askari na jamii kwa ujumla wanapaswa kufanya mazoezi pale
wanapopata nafasi na sio mpaka walazimishwe kwani mazoezi yanasaidia kujenga
mwili na kuuepusha mwili na magonjwa kama vile presha na kisukari,” amesema,
Awali Kamanda Mambosasa aliwapongeza askari kwa kushiriki
mazoezi hayo, amesema mazoezi hayo yatakua endelevu kwa askari wote wa polisi
kanda maalum ya Dar es Salaam .
Matembezi hayo ya root match yalifanyika katika mikoa ya kipolisi
Temeke na Kinondoni na yatakuwa yakifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
No comments:
Post a Comment