Makonda ateuliwa tena...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewateua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na mkurugenzi mkuu wa makampuni ya Bakhresa Limited, Abubakar Bakhresa kwenye kamati za maandalizi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17) yatakayofanyika 2019 nchini.


Rais wa TFF Wallace Karia

Katika uteuzi huo Makonda ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya miundombinu huku Bakhresa akiteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa  kamati ya usafiri na malazi.

Kwa mujibu wa rais wa TFF, Wallace Karia, Makonda atasaidiwa na makamu mwenyekiti Yusuph Singo ambaye pia ni mkurugenzi wa michezo.

Wajumbe katika kamati ya miundumbinu ni Sunday Kayuni, Leslie Liunda, Nassoro Idrissa ‘Father’, Mohamed Kiganja katibu wa baraza la michezo la taifa (BMT) na Mhandisi Davis Shemangale.

Kwa upande wake Bakhresa atakuwa chini ya mwenyekiti mhandisi Ladislaus Matindi na wa kamati hiyo ni  Aziz Abood, Ahmed Mgoyi, Ahmed Shabiby, Dk. Maige Mwakasege Mwasimba na Shebe Machumani.

TFF pia imeunda kamati ya masoko na mabari chini ya Mwenyekiti, Kelvin Twissa na Wajumbe Mwandishi wa Habari za Michezo na Katibu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas, Dk. Omari Swaleh wa  Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkurugenzi wa AMG Group Iman Kajula na Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando.

Kamati nyingine ni ya Fedha na Mipango itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Doto James na Wajumbe Mohamed Dewji, Dk. Seif Muba, Bernard Lubogo, Paul Bilabaye, Jacquelline Woiso na Cornel Barnabas.

Kamati ya Uratibu Utalii itakuwa chini ya Mwenyekiti, Dk Khamis Kigwangala na Wajumbe , Allan Kijazi Devotha Mdachi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke, Hoyce Temu, Leah Kihumbi ambaye ni Mkurugenzi wa Sanaa na Makamu Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani.

Kamati ya Itifaki, Mwenyekiti ni Mndolwa Yusuph ambaye ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Wajumbe Filbert Bayi, Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA, Happiness Luangisa, Alex Makoye Nkenyenge na Alhaji Idd Mshangama.

Kamati ya Tiba na Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli itakuwa chini ya Mwenyekiti, Profesa Lawrence Museru, Dk. Paul Marealle, Dk. Edmund Ndalama, Dk. Christina Luambano, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke na Hiiti Sillo.
Kamati ya Sheria na Taratibu Mwenyekiti ni William Erio na Wajumbe Dk. Damas Ndumbaro, Edwin Kidifu, Ally Mayai na Khalid Abeid.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mwenyekiti ni  IGP Simon Siro na Wajumbe Michael Wambura, CP. Andengenye wa Zimamoto, CP. Lazaro Mambosasa wa Polisi Kanda Maalum ya Dar-es-Salaam, Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani, TISS na Jonas Mahanga.

Kamati ya Rasilimali Watu itakuwa chini ya Mwenyekiti Dk. Francis Michael, Allan Kijazi, Wane Mkisi, Juliana Yassoda na Gerald Mwanilwa.

Kamati hizo ndogo zitakuwa chini ya Kamati Kuu inayoongozwa na Mwenyekiti Dk. Harrison Mwakyembe (MP); Makamu Mwenyekiti wa Leodegar Tenga na Mtendaji Mkuu wa Kamati hiyo ni Henry B. Tandau.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search