Mamilioni ya dola yaliibwa katika mazishi ya Mandela...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
MIAKA minne tangu kufarika kwa aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika kusini, Nelson
Mandela imebainika viongozi wakuu nchini humo wanadaiwa kufanya ufisadi mkubwa
katika mazishi ya kiongozi huyo.
Hayati Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini
Mamlaka ya kupambana na
rushwa nchini humo imebaini kuwa takriban dola milioni 22 ilitumika vibaya
wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka minne iliyopita.
Ripoti hiyo inasema kwamba
viongozi hao walifuja pesa na kukiuka taratibu zilizowekwa huku ikisemekana
kwamba gharama za bidhaa ziliongezwa maradufu na matumizi mazishi kutajwa kuwa
ya juu sana kwa mfano shati za kumbukumbu ya mazishi zilinunuliwa kwa dola 25
badala ya dola 19 .
Hata hivyo ripoti hiyo
imetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliofanya jambo hilo la
kushangaza katika jamii.
No comments:
Post a Comment