Waziri Kalemani :Hakuna mgawo wa umeme...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu
WAZIRI wa Nishati, Dk
Medard Kalemani amesema hali ya umeme
kwa sasa ni wastani na hakuna mgao.
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani
Amesema hayo katika
kipindi cha tunatekeleza na kusema “ Si
kwamba tuna mgao wa umeme, tunarekebisha mitambo ya umeme iliyodumu kwa
takribani miaka 40.”
Amesema lengo ni
kuhakikisha kunakuwapo na mitambo ya umeme itakayowezesha kutoa huduma ya umeme
kwa uhakika na kuwa umeme
ni uchumi na huwezi kutenganisha masuala ya maendeleo na nishati.
Waziri hiyo amesema
upungufu wa umeme unatokana na ukarabati unaoendelea na mafundi hawalali
kuhakikisha hali inakuwa sawa.
“Hadi kufikia Desemba 15,2017 tutakuwa tumefanya
ukarabati katika sehemu kubwa na kutakuwa na tofauti kubwa,’’ amesema
Pia amesema hadi kufikia mwezi wa 1 au wa 2, 2018 mkandarasi wa
kujenga stiegler's gorge atapatikana
na kuanza ujenzi. Mradi wa stiegler's gorge utazalisha megawati 2100 kwa
mkupuo.
Amesema mradi wa Kinyerezi 2 umekamilika kwa 86% na
kuanzia mwezi huu utaanza kutoa megawati
30 kila mwezi.
Mradi wa umeme Makambako-Songea ni mradi mkubwa
utakuwa na vituo 3 vya kupoozea umeme, utakamilika Septemba mwakani.
Waziri huyo amesema katika REA 3 serikali itahakikisha
kila kijiji kinapata umeme na kwamba vijiji zaidi ya 7,000 havijapata umeme
"Mpaka kufikia mwaka 2021
vijiji vyote vitakuwa vimepata umeme,’’ amesema
No comments:
Post a Comment