Mandozi kufungua kijiji cha michezo Misungwi..soma habari kamili na matukio360..#share

Na Mwandishi Wetu

KITUO cha Michezo cha Mandozi Sport Academy kinatarajia kufungua kijiji cha michezo Januari 3, 2018 kitakachokuwa Sumve wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Wachezaji wa kituo cha michezo cha mandozi sport academy wakifanya mazoezi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo hicho Mohamed Ngaiza wakati akizungumza namwandishi wa habari hii kwa njia ya simu kutoka Mwanza.

Ngaiza amesema wamelazimika kufungua kijiji hicho ambacho kitaweza kuchukua watoto zaidi ya 20 kwa pamoja ili kuweza kukuza vipaji vya vijana ambao wanashiriki mchezo wa mpira nchini.

Amesema kwa sasa wanatarajia kijiji hicho kitachukua vijana hao 20 huku matarajio yakiwa ni kuhakikisha kuwa wanachukua vijana 50 wa rika mbalimbali kuanzia miaka 8 hadi 20.

“Mandozi Sports Academy ni kituo ambacho kimeanzishwa miaka mine iliyopota na matarajio yetu ni kuhakikisha kuwa vijana wenye vipaji vya mpira wanapata msingi mzuri na matunda yameshapatikana kwani tumewatoa Selemani Hamisi wa Ruvu Shooting na Pius Buswita wa Yanga,"amesema.

Meneja huyo amesema matarajio yao ni kuona kijiji hicho kutoa vijana ambao watakuwa na ujuzi mbalimbali ikiwemo kucheza mpira, kujifunza maisha ya ujasiriamali na kusoma.

Ngaiza amesema katika kuhakikisha vijana hao wanaishi katika misingi ya kisheria na nidhamu wanawapatia mikataba ya kisheria ili kuepuka ulaghai ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara kwa wachezaji wao.

Aidha amesema wamefanya mawasiliano na wakala na vilabu mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanauza wachezaji wao kwa kufuata misingi na taratibu za kisheria.

“Tumewasiliana na Alex Kajumulo yupo Marekani, Rwanda tuna wakala, pia klabu ya Azama na Kagera Sukari tumekubaliana kushirikiana naamini siku moja Mandozi itakufanikiwa,” amesema.

Amesema malengo makubwa ni kuuza wachezaji wankidhi sifa ili kuruhusu vijana wengine wenye vipaji kuingia kuonesha vipaji vyao.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search