Nikol yawakumbuka wanahisa wake...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu

Kampuni ya uwekezaji ya Nicol imeazimia kutoka gawio la Sh 25 kwa kila hisa kwa kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Desemba 31,2016 kwa wanahisa wake na kwamba  gawio hilo lilipwe kuanzia  Februari 28, 2018.
Mwenyekiti wa Nicol, Dk Gideon Kaunda
Ni kutokana na faida  iliyopatikana baada ya kodi  ya mwaka 2016 ya Sh 8.67 bilioni.
Kampuni ya Nicol kwa miaka 10 ili kuwa  haijatoa gawio kwa wanahisa wake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Bodi ya Nicol, Dk Gideon Kaunda katika mkutano mkuu wa tatu wa mwaka wa Wanahisa wa Nicol uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

Mkutano huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu namba 54 cha kanuni za kampuni hiyo baada ya akidi ya wanahisa wanaomiliki theluthi moja ya his a zilizotolewa na kulipiwa kutimia.

Pia Nicol inategemea kurudi katika solo la Hisa la Dar es Salaam kabla ya mwezi Aprili, 2018.

Pia alitaka ukaguzi wa kitaalam (forensic audit ) unaendelea ukamilishwe haraka iwezekanavyo na matokeo yake yawekwe bayana kwa madhumuni ya kuchukua hatua dhidi ya wahusika.

Mgeni rasmi, Balozi Dr  Matern Lumbanga Alisema Nicol sasa imechukua sura mpya kwa kufanya mambo ambayo yanaleta matumaini  hayakuwepo kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Alisema ni kutokana na kuonekana kuimarika kwa Mali za kampuni kwa kuongezeka kutoka Sh 23.4 bilioni mwaka 2010 mpaka kufikia Sh 94 bilioni mwaka 2015.

Mapato kutokana na uwekezaji yaliongezeka kutoka Sh 1 bilioni 2010 mpaka kufikia Sh 3.7 bilioni  mwaka 2015.

Kutoka mwaka 2010 mpaka 2015 Nicol ilitengeneza faida kila mwaka, thamani ya  hisa ilipanda kutoka Sh 344 milioni  mpaka kufikia Sh 2.2 bilioni mwaka 2015.

Alisema kwa matokeo hayo, aliwapongeza wajumbe wa bodi ya Nicol na pia aliwasihi waitunze Nicol kwa faida yao.

Jaji Mark Bomani alipendekeza Nicol izaliwe upya na mambo Mabaya yaliyofanyika huko nyuma yasahaulike.

" Kwa kuwa waliofungua kesi hawakujua walichokuwa wanatenda ama walikuwa na niambaya hivyo sisi tuanze na nia nzuri, tujione kama tumeokoka."

Tujipange upya kamati ya mipango ijipange upya iwekeze katika makampuni ambayo yatatoa faida kwa wanahisa na siyo yatakayowapa hasara.

Sisi tuanze na nia nzuri tusonge mbele  na kupendekeza hilo gawio liwe angalau liwe Sh 50 kwa kila hisa na kwamba hilo linawezekana.

Alisema Nicol ina zaidi ya miaka 10 haina gawio kwa wanahisa wake na kwamba gawio hilo litarejesha imani kwa wanahisa na kuwavutia wanahisa wapya.
Mwisho








About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search