Mbunge Lijualikali na Susan Kiwanga waendelea kusota rumande..soma habari kamili na matukio360...#share
PETER Lijualikali na Suzan Kiwanga wabunge wa Kirombelo na Mlimba wote
kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wenzao 36 wamerejeshwa
rumande.
P Lijualikali na Suzan Kiwanga
Wabunge hao na wenzao leo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi
Morogoro ambapo mahakama ilitakiwa kutoa uamuzi wa dhamana lakini umekwama kutokana
na kuibuka hoja za kisheria.
Kulitokea mvutano kati ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kuhusu
hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.
Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo
hadi kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu
hoja kuhusu hati hiyo.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi
ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick
Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki
na Sunday Hyera.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama
hicho, Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani.
Wengine waliofika mahakamani ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na
wa Viti Maalumu, Devota Minja.
No comments:
Post a Comment