Mume, mke kizimbani kwa Heroin gram 375...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
MUME na mke ambao ni
wafanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin gram 375.20.
Akisoma hati ya mashtaka leo
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Wakili wa Serikali, Adolf Mkini
amewataja washtakiwa hao kuwa ni Minda
Mfamai, mkewe Fatuma Mpondi na mwenzao Oswini Mango.
Wakili Mkini amedai Novemba
22, 2017 katika maeneo ya Chamazi kwa Mkongo Mbagala, wilayani Temeke, Dar es Salaam washtakiwa hao walisafirisha
madawa hayo.
Baada ya kusomewa shtaka
hilo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu
chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya
kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Hakimu Mashauri ameiarisha
kesi hiyo hadi Desemba 19,2017 na kuamuru mshtakiwa Minda akatibiwe baada ya kulalamika
kuwa alipigwa alipokuwa polisi.
No comments:
Post a Comment