Wanaotumia ARvs Dodoma waongezeka... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dodoma
TAKRIBANI
wagonjwa kati ya 100 hadi 1200 wanaotumia
dawa za kufumbaza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi(ARvs) mkoani Dodoma,
kwa siku hupokea dawa hizo.
Pia idadi ya wanaotumia dawa hizo imeongezeka kutoka wagonjwa 3,144 hadi 6,244. Kati ya hao wanawake ni 4876.
Waziri wa afya, Ummy Mwalimu
Mtakwimu wa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Venance Makuza ameiambia
matukio360 kuwa takwimu hizo ni za kipindi cha April hadi Septemba 2017.
Amesema ongezeko hilo ni kutokana na mwamko wa jamii kupima afya hususan wageni
wanaoingia na kutoka katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
“Kwa siku tunatoa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi(ARvs)
kwa wagonjwa 100 hadi 1200 licha ya
wengine kutoudhuria kliniki kwa sababu zisizokuwa za msingi za mila, desturi na
Imani za kidini,’’ amesema
Mkuu wa kitengo cha
maambukizi mpya ya virusi vya Ukimwi (HIV) mkoani humo, Dk Silaji Shaban
amesema idadi kubwa ya wanawake ni
kutokana na mwamko wao wa kujitokeza
kupima afya na kupata ushauri nasaha.
"Pamoja na mambo mengine changamoto tunayokabilina
nayo ni baadhi ya wagonjwa kuacha tiba kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa tendo la ndoa na imani za kidini, mira
na destuli ,"amesema
Katika hatua nyingine Dk Shaban ameonya wagonjwa
wanaotumia(ARvs) kuacha tabia ya ulevi wa pombe na kwamba inachangia usugu wa dawa
na hatari ya kupata ugonjwa wa ini
Msimamizi wa kitengo cha utoaji dawa za ARvs,
Sylvester Lugia amesem elimu ya uhamasishaji jamii kupima afya inabidi
iongezeke na waathirika kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya ili kuongeza
siku za kuishi.
No comments:
Post a Comment