Mfumuko wa bei nchini wapungua...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu
MFUMUKO wa bei mwezi Novemba, 2017 umepungua
hadi asilimia 4.4 ikilinganishwa na asilimia 5.1 mwezi
Oktoba, 2017.
Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii kutoka ofisi ya taifa ya takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii kutoka ofisi ya taifa ya
takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa mwezi
Novemba, 2017 kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za
vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Novemba, 2017 ikilinganishwa na bei za
mwezi Novemba, 2016.
“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa
mfumuko wa bei ni nyama ya ng’ombe asilimia 5.4, samaki wabichi asilimia 22.2, mbogamboga asilimia 3.9, viazi mviringo asilimia
14.0, mihogo mibichi asilimia 24.8 na viazi vitamu kwa asilimia 13.4,”
amesema.
Amesema mfumuko wa bei nchini unamwelekeo unaofanana na baadhi
ya nchi nyingine za Afrika Mashariki, nchini Kenya mfumuko wa bei mwezi
Novemba, 2017 umepungua hadi asilimia 4.73 kutoka asilimia 5.72 mwezi Oktoba,
2017 na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.0 mwezi Novemba, 2017 kutoka
asilimia 4.8 mwezi Oktoba, 2017.
No comments:
Post a Comment