Rugemarila ataka mwizi bilioni 309 abainishwe...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
JAMES Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji wa
fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji ushirikiano
baina yake na upande wa mashtaka ili kubaini mwizi wa bilioni 309 za serikali.
James Rugemarila wa kwanza kushoto
Ameyasema hayo leo umbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru,
Leornad Swai kudai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado
haujakamilika.
Pia Rugemarila amedai
hajawahi kupata nafasi ya kuzungumza na mawakili wake tangu alipotoka mahakama
tarehe iliyopita.
Hivyo anashindwa kupata
ushauri, wala hajui nini kinaendelea kuhusu kesi yake, hivyo ameomba waruhusiwe
mawakili wawili badala ya kumi ili wawe wanamuelezea kuhusu mwenendo wa kesi.
Awali kabla ya kutoa hoja hizo,
wakili wa utetezi Balomi amedai suala la
upelelezi katika kesi hiyo linachelewesha na kuwa linakiuka misingi ya haki ya
kikatiba kwa washtakiwa.
Balomi amedai kuwa ni miezi
6 sasa, tunaambiwa upelelezi haujakamilika, Wakili wa serikali anashindwa hata
kutuambia umefikia wapi na umebaki muda gani kukamilika.
Pia wakili Balomi amedai
hali ya washtakiwa kiafya sio nzuri hasa Sethi, hivyo upelelezi ukamilishwe kwa
haraka ama wawe wanaelezwa hatua ulipofikia.
Akijibu hoja hizo Wakili
Swai alidai upande wa utetezi ndio umekuwa ukikwamisha mchakato wa upelelezi
kwani wamekuwa wakiwanyima baadhi ya nyaraka.
Swai amedai kuwa anashukuru
wanaelewa kwamba upelelezi ni mchakato na katika kuonyesha hilo wiki iliyopita walifanya
mahojiano na washtakiwa licha ya kuwa mshtakiwa Seth aliwanyima ushirikiano.
Pia Swai amedai kuwa
kuchelewa kwa upelelezi huo kunasababishwa na ushahidi mwingine kuwepo nje ya
nchi.
Baada ya kueleza hayo,
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 22, 2017 ambapo ameutaka
upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi.
Mbali ya Rugemarila,
mshtakiwa mwingine ni Harbinder Singh Sethi ambapo wanakabiliwa na mashtaka 12
ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya USD 22, 198,544.60
na bilioni 309
No comments:
Post a Comment