Mjema:Ukimwi changamoto kufikia sera ya viwanda...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema janga la Ukimwi
bado ni changamoto katika kufikia sera ya viwanda nchini.
Mkuu wa wilaya Ilala Sophia Mjema akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani jijini Dar es Salaam.
Mjema ameyasema hayo jana wakati wa kelele cha siku ya ukimwi
duniani.
Amesema janga hilo ni matokeo ya mchanganyiko wa sababu nyingi
za kibaiolojia, Kijamii, kimila na kiuchumi.
"Madhara ya Ukimwi yameadhiri watu binafsi familia na jamii
kwa ujumla hivyo udhibiti wake unahitaji nguvu za pamoja za wananchi na wadau
wa maendeleo, asasi za kiraia, sekta binafsi, taasisi za dini na serikali,
"amesema.
Amesema mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa mikoa yenye
changamoto nyingi katika kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi.
Mjema amesema mkoa huo umekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu
kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Amefafanua kuwa mbali na mwingiliano huo, kiwango cha maambukizi
kimeendelea kushuka kutoka asilimia 9.3 hadi asilimia 6.9 kwa mwaka 2007 hadi
2012.
"Haya ni mafanikio makubwa ya kujivunia. Hatutakiwi kubweka
na mafanikio haya na kujisahau kwani kunaweza kusababisha kiwango hiki cha
maambukizi kupanda tena, "amesema.
Ameongeza kuwa jitahidi zinatakiwa kuchukuliwa ili maambukizi
yaendelee kushuka ili kufikia lengo la kumaliza kabisa ukimwi ifikapo
2030.
Mjema ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuchukua tahadhari na
kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kufika 0 mkoani humo na
kujiepusha na tabia hatarishi.
"Hadi Oktoba 2017 watu waliopima virusi vya ukimwi na
kupokea majibu ni milioni 1.3, wanaume 52953 sawa na asilimia 37 na wanawake
87770 sawa na asilimia 63,"amesema.
Amesema waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi walikuwa
42695 ambapo wanaume ni 16950 sawa na asilimia 40, wanawake wakiwa 25745 sawa
na asilimia 60.
Amesema jumla ya maambukizi kwa mkoa huo ni asilimia 3.0
ukilinganisha na takwimu za mwaka 2011/2012 inaonesha kupungua kwa maambukizi
mapya.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana na ajira, Jenista Mahagama amemtaka Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi(TACAIDS) , Dk. Leonard Maboko
kuanzisha kampeni maalumu ya wanaume kupima ukimwi hapa nchini 2018.
"Bado kunatatizo la mwitikio wa wanaume kujitokeza na
kupima virusi vya ukimwi... Mwaka 2018 namuagiza aandae kampeni maalumu ya
kuwahamisisha wanaume wote kupata nafasi ya kupima virusi vya ukimwi,
"amesema .
Amesema itasaidia kuendelea na mwitikio wa mapambano ya ukimwi
huku akiwasihi wanawake kuendelea kuwa mstari wa mbele kupima na kujua afya
zao.
No comments:
Post a Comment