Mjue kiongozi mpya wa ANC....soma habari kamili na matukio360..#share
Na mashirika ya kimataifa
CHAMA tawala nchini Afrika
Kusini kimemchagua Cyril Ramaphosa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho.
Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa
Ramposa ambaye alikuwa
makamu wa rais wa chama hicho aliweza kumshinda mpinzani wake Nkosazana
Dlamini-Zuma, ambaye ni waziri wa zamani na alikuwa mke wa rais Zuma kwa kura
2440 kwa 2161.
Kwa sasa Ramaphosa ameoneka
kuwepo kwenye nafasi kubwa ya kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2019.
Hata hivyo Cyril Ramposa
amekuwa kiongozi wakati ambao Afrika kusini inakabiliwa na changamoto nyingi
ambazo zinafanya mambo hayendi sawa katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa
barani Afrika .
Cyril
Ramaphosa ni mtu wa aina gani?
Cyril Ramposa alizaliwa
tarehe 17 mwezi novemba mwaka 1952 mjini Soweto, ndio mwanasiasa tajiri zaidi
Afrika Kusini ,utajiri wake unakisiwa kuwa ni dola milioni 450.Tangu ujana wake
Ramposa alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa shupavu na hiyo ndio ilimfanya kujiunga
na uongozi wa chama cha wafanyakazi
Na wakati chama cha ANC
kilipochukua uongozi wa Afrika kusini mwaka 1994,alitamani sana kuwa naibu wa
mwasisi wa Afrika Kusini mpya ,Nelson Mandela lakini pale Mandela alipompuuza
na badala yake kumteua Jacob Zuma inasemekana kuwa bwana Ramaphosa alisusia
hata sherehe za kuapishwa kwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini vilevile
alisusia kuchukua wadhifa wowote wa uongozi katika serikali mpya ya Afrika
Kusini .
Jacob Zuma na makamu wake
walazimishwa kusalimiana
Badala yake bwana Cyril
Ramaphosa ambaye alisomea uwakili alihiari kuwa mbunge na mwenyekiti wa bunge
la katiba ambalo lilishughulikia kutengeneza katiba ambayo ilisifiwa sana
duniani.
Badaye Ramaphosa alishangaza
wengi alipojiuzulu kutoka kwenye siasa na kushughulika zaidi katika biashara
zake,lakini mwaka 2012 alishawishika tena na kurudi kwenye siasa na kuwa na
ilipofika mwaka 2014,alipanda zaidi na kuwa makamu wa rais Zuma.
Na wachambuzi wa masuala ya
kisiasa wanasema kurudi kwake Ramaphosa kwenye chama cha ANC kulirudisha imani
ya wananchi wengi licha ya kuwa chama hicho kilikuwa kinakabiliwa na kashfa
nyingi za kisiasa.
No comments:
Post a Comment