Everton yazidi kuchanja mbuga, Rooney afanya yake...soma habari kamili na matukio...#share
Na mashirika ya kimataifa
KLABU ya Swansea City imekubali kipigo cha magoli 3-1
kutoka kwa Everton katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Goodsoonpark.
Wachezaji wa Everton wakishangilia goli
Baada ya kupoteza mchezo huo
Swansea wanaendelea kuburuza mkia wakiwa
na alama 12, wakiwa wamecheza 18.
Kunako dakika ya 35 kipindi
cha kwanza Swansea ndio walianza kuzifumania nyavu za Everton kwa goli Leroy
Johan Fer.
Katika dakika ya 45,
mshambuliaji kinda wa Everton Dominic Calvert-Lewin akasawazisha goli hilo
baada ya mkwaju wa penati ya Wayne Rooney kuokolewa.
Kiungo Gylfi Sigurdsson
akaongeza goli la pili katika dakika ya 64, Wayne Rooney akasawazisha makosa
yake kwa kufunga goli la tatu kwa mkwaju wa penati na kufikisha jumla ya magoli
10, msimu huu.
No comments:
Post a Comment