Mkuu wa wilaya aonya wafanyabiashara....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu
MKUU wa wilaya ya Mbeya, Poul Ntinika ameonya wafanyabishara wanaokaidia agizo la serikali la kuendelea
kuuza pombe na vyakula kwa kujificha kufuatia kufungiwa kutokana na kuwapo kwa ugonjwa wa kipindupindu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Poul Ntinika (kulia) akinunua ndizi kutoka kwa mfanyabishara ambaye akutaja jina lake katika soko la Maghorofani kata ya Uyole (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Amos Makalla.
Ntinika amesema walilazimika kufunga biashara kwenye vilabu vya pombe za kienyeji na mama lishe
kufuatia kuwapo kwa mgonjwa aliyekuwa na
dalili za kipindupindu.
Kata zinazokabiliwa na changamoto hiyo ni Mbalizi road, mabatini, simike na mamlaka ya
mji mdogo wa Mbalizi.
"Watu hawaelewi kuna dalili za kuwepo ugonjwa wa kipindupindu
na tumebaini kuna wafanyabishara wanakaidi agizo la serikali sasa nimewaagiza
watendaji ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao."amesema
Ntinika amewataka wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na
magonjwa yanayoepukika na kuboresha afya zao.
Diwani wa kata ya Mbalizi Road, Adam Hussein, (CCM)
amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuzingatia kanuni bora
za afya
Mwenyekiti wa mtaa wa Mwasyoge kata ya Mbalizi road,
Noah Mwakafwila amesema zoezi la kufuatilia wafanyabishara wanaouza vyakula na pombe kwa siri litaanza.
Amesema sera ya usafi ni kipaumbele chake na kwamba kila kaya
inawajibu wa kutekeleza hilo.
Hata hivyo mfanyabishara wa vileo, Sarah Braison ameiomba
serikali kuwafungulia kwa kuwa idadi kubwa wanamikopo na sasa wanakosa fedha za marejesho hali inayoweza kukimbia na kutelekeza
familia zao.
No comments:
Post a Comment