Mwakyembe kushuhudia Simba ikipata mmiliki mpya ...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu
WAZIRI wa Habari, utamaduni, Sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe kesho anatarajia kushuhudia klabu ya Simba ikiweka historia pale itakapomtangaza mzabuni aliyeshinda kuimiliki kwa asilimia 51.
Kikosi cha Simba Sc.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesem kuwa Dk. Mwakyembe anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu ambao utamtangaza mshindi wa umiliki wa klabu.

"Simba SC imekuwa na sifa nyingi ndani na nje ya uwanja. Moja ya sifa kuu ya Simba SC ni uwezo wa wanachama, mashabiki na wapenzi wake kukubaliana na mabadiliko chanya,"

"Ikiwa imeanza mchakato wa ubadilishaji wa uendeshaji na umiliki, kesho ni siku kubwa kwa Simba ambapo mzabuni aliyeshinda kumiliki sehemu ya klabu hii atatajwa kwenye Mkutano Mkuu maalum," imesema.

Mkutano huu utaonyeshwa live kwenye kurasa za Simba SC

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search