Serikali yataja siri kumi kufanikiwa katika ujasiliamali ...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
KATIBU tawala mkoa wa Dar es Salaam(RAS),Theresia
Mbando ametoa siri kumi kwa wajasiliamali kufanikiwa na kukuza uchumi nchini.
Katibu tawala(RAS) mkoa wa Dar es Salaam,Theresia Mbando akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa na wajasiliamali jijini Dar es Salaam.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tano
kwa wakufunzi na wajasiliamali 73 kutoka mikoa mbalimbali ikiwamo Tanga,
Njombe, Morogoro, Shinyanga, Singida na Dar es Salaam yaliyotolewa na Shirika
la Viwanda Vidogo (SIDO).
Amesema miongoni mwa siri hizo ni ujasiri wa kuthubutu
na kuchukua tahadhari ya kupata hasara bila kukata tamaa.
Ya pili ni malengo ya muda mrefu na mfupi yatakayowaongoza
katika utendaji na sababu ya tatu ni kutafuta
na kufuata taarifa zinazohusu ujuzi.
"Mkazalishe wajasiliamali na kutengeneza bidhaa
bora ili zikidhi viwango vya soko la ndani na nje,"amesema.
Katibu tawala huyo amesema sababu ya tano ni kufanya biashara kwa kujiamini na kutafuta
mianya iliyowazi kwa wateja. Sababu ya sita kuheshimu mikataba ya kazi kwa
wateja inayoendana na bidhaa zao.
Sababu ya saba ni kuwa na uwezo wa kushawishi wateja
na si kumwona mteja anashida. Ya
nane uvumilivu.
"Sababu ya tisa ni mtengeneze bidhaa zinazokidhi matarajio ya
walaji hii itasaidia kuwaongezea kipato, "amesema.
Amesema wajasiliamali wanapaswa kupokea ushauri kutoka
kwa wateja, wataalam na kuifanyia kazi na kuendesha biashara katika mfumo rasmi
ili kuepusha hasara.
Amesema mbali na siri hizo wanapaswa kufuata utaratibu
na matakwa ya serikali kuwa na leseni pamoja na kuthibitishwa na shirika la
viwango (TBS).
Meneja wa SIDO mkoani Dar es Salaam, MacDolnard Maganga
amewaasa wajasiliamali kuweka
vifungashio vinavyovutia ili kuvutia wateja.
"Kama kifungashio si
kizuri hakina mvuto hakuna mnunuzi atakayenunua ni lazima viwe na ubora,
"amesema.
No comments:
Post a Comment