Waarabu wamtunishia misuli Donald Trump....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
WAZIRI wa mashauri ya nchi
za kigeni wa Lebanon, Gebran Bassil amesema mataifa ya kiarabu, yanafaa kufikiria hatua ya
kuiwekea Marekani vikwazo vya kiuchumi ili kuizuia kuhamishia makao makuu ya
Israeli hadi Jerusalem, kutoka Tel- Aviv.
Pia Bassil amesema hatua za
kidiplomasia na kisiasa, zinafaa kuchukuliwa, kisha kufuatiwa na vikwazo vya
kiuchumi na kifedha.
Rais wa Marekani, Donald Trump
Ametoa msimamo huo katika
mkutano wao mjini Cairo-Misri.
Taarifa walioitoa kwa kauli
moja kwenye mkutano wao Mjini Cairo- Misri, muungano huo wa waarabu umesema kuwa hatua ya Marekani
kuutambua mji wa Jerusalem kama makao
makuu ya Israel ni hatari na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, na
litaitumbukiza mataifa ya mashariki ya kati katika ghasia mbaya.
Mawaziri kwenye mkutano huo,
sasa wanaiomba jamii ya kimataifa kutaja Mashariki mwa Jerusalem kama makao
makuu ya Palestina.
Kumeshuhudiwa tena ghasia
katika ukanda wa Gaza na maeneo ambayo yanashikiliwa na Israeli, Magharibi mwa
mto Jordan.
No comments:
Post a Comment