Serikali yatakiwa kuwasaidia wakandarasi wazawa...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Salha Mohamed,Dar es Salaam
WADAU wa ujenzi nchini wameiomba serikali kuwashinikiza wakandarasi wageni wanaofanya miradi mikubwa nchini kushirikiana na wazawa katika ujenzi wa miradi mikubwa ili wapate ujuzi na uzoefu.
Mkutano wa wadau wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam
Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi(NCC),Matiko Mturi ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa ujenzi, wakandarasi, wahandisi, wasanifu majengo na wanaofanya kazi katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
"Ujuzi upo, lakini baadhi ya miradi inavyozidi kuwa mikubwa ujuzi unaongezeka.
Amesema changamoto wanayokumbana nayo ni kutokuwa na uzoefu katika ujenzi wa miradi mikubwa kama wa reli kwa kiwango cha standard gauge.
"Changamoto kubwa ni kutokuwa na ujuzi na uzoefu katika hayo maeneo, hivyo tunataka kuangalia namna gani serikali inaweza kuwezesha wageni wanaokuja kutekeleza miradi hiyo kuwawezesha watanzania kupata ujuzi,"amesema.
Amesema mbali na kupata uzoefu, kupata mafunzo yanaweza kusaidia watu kuelewa namna ya kusimamia miradi mikubwa kama hiyo kwani imeonekana kuwa na mambo mengi inayohitaji uzoefu, elimu na ujuzi.
"Tumewaita hapa watuambie vitu gani serikali ivifanyie kazi ili kuwajengea uwezo katika miradi inayokuja kutekelezwa, "amesema.
Amesema wasambazaji wa malighafi wanapata changamoto ya ushindani na wanaoingiza vifaa kutoka nje ya nchi hivyo kupitia mkutano huo utawezesha na kuongeza ubora wa vifaa vyao ili vitumike katika miradi ya hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elizabeth Tagora amesema kupitia mkutano huo wanaimarisha baraza la ujenzi litakaloleta tija nchini.
"Baraza la ujenzi lisiposimamiwa vema inamaana halitasimamia vema sera yetu ya ujenzi, kwani inatakiwa isimamiwe utekelezaji wake na kufikia lengo, "amesema.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment