Watoto sita wapelekwa Israel kutibiwa moyo...soma habari na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya okoa moyo wa mtoto (Save a
Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka watoto sita wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka kumi na tatu nchini Israel kwa
ajili ya matibabu ya moyo.
Taarifa
iliyotolewa leo na kitengo cha uhusiano na masoko cha JKCI, imesema watoto hao
wamesafiri jana alifajiri wakiwa na wazazi wao pamoja na wauguzi.
Baada ya matibabu
ya watoto kukamilika maafisa wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya
kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo
katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.
“Taasisi
yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto kupitia
wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya
wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa
ajili ya matibabu,” imesema.
“Tunaushirikiano
mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa
na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya
kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita
na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu
wagonjwa katika taasisi yetu,”.
Daktari mmoja wa JKCI bado anaendelea na masomo nchini humo.
Hilo ni kundi la tano
la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015
ambapo JKCI ilianza ushirikiano na taasisi ya okoa moyo wa mtoto (Save a
Child’s Heart –SACH) ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo.
Hadi sasa watoto 46
wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.
Taasisi imeendelea
kutoa wito kwa wazazi na walezi kupima afya za watoto wao ili kuweza kubaini
kama kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo
yanaanzia utotoni.
Mtoto akianza
kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya
kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa
mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.
No comments:
Post a Comment