Waliotaka kusafirisha madini bilioni 1.5 wapandishwa kizimbani...soma habari kamili na matukio360..#share
Na Abdulrahim Sadiki
MFANYABIASHARA Naushad
Mohammed Suleiman (63) na Ali Makame (36) wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha madini ya dhahabu vipande saba
vyenye thamani ya bilioni 1.5 bila ya kuwa na leseni
Wamesomewa makosa yao leo
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa serikali, Jehovanes
Zacharia.
Wakili Zacharia amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa
mawili ikiwemo la uhujumu uchumi.
Wakili Zacharia amedai
katika shtaka la kwanza la kula njama
kuwa washtakiwa hao walitenda shtaka
hilo tarehe tofauti kati ya Novemba mosi
na 29, 2017.
Amedai katika tarehe hizo washtakiwa hao wakiwa
maeneo ya Geita Mjini na Dar es Salaam walikula njama na watu wengine ambao
hawakufikishwa mahakamani ili wasafirishe madini ya dhahabu nje ya nchi bila ya
kuwa na Leseni.
Pia wanadaiwa kusafirisha madini bila ya kuwa na kibali,
inadaiwa kuwa walitenda shtaka hilo
Novemba 29,2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume
Zanzibar.
Ambapo walikutwa wakisafirisha madini ya dhahabu
vipande saba vikiwa na uzito wa Kilo.18.354 yakiwa na thamani ya Sh
1,505,009,929.38.
Baada ya kusomewa mashtaka
yao, Hakimu Mashauri amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu kitu chochote kwa
sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Wakili Zacharia amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo namba 81 ya mwaka
2017 bado haujakamilika na kesi
imeahirishwa hadi
Desemba 20,2017.
No comments:
Post a Comment