Wanawake waliovaa suruali wakamatwa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
WANAWAKE 24 wa Sudan
wameshtakiwa kwa kujivunjia heshima, baada ya kuonekana wamevaa suruali katika
karamu moja mjini Khartoum.
Baadhi ya wanawake wakiwa wamevaa suruali
Karamu hiyo ilivamiwa na polisi
wa nidhamu wiki iliyopita.
Suruali zinachukuliwa na
wakuu kuwa vazi la utovu wa adabu, na adhabu yake ni mijeledi 40 pamoja na
faini.
Wanaharakati wanasema maelfu
ya wanawake wanakamatwa kila mwaka, na kuchapwa mijeledi.
Wanasema sheria inayopiga
marufuku suruali na sketi fupi na za kubana, inawabagua wakristo, na inatumiwa
kiholela. Kawaida wanaweke nchini Sudan
huvaa nguo ndefu.
Katika suala la mavazi kila
nchi inauamuzi wake nchini Austaria mavazi ya niqab na burka yamepigwa marufuku
No comments:
Post a Comment