ACT Wazalendo watoa neno uchaguzi Kinondoni, Siha...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
WAKATI chama cha Chadema kikibadilisha msimamo wake, chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea na msimamo wake wa kutoshiriki kwenye uchaguzi
mdogo wa ubunge katika jimbo la Siha na Kinondoni, utakaofanyika Februari 17,2018
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.
Hivi karibuni Chadema ilitangaza wagombea katika majimbo hayo ikiashiria kutengua
msimamo ambao walikuwa nao awali wa kususia uchaguzi mdogo wa marudio hadi hapo NEC itakapokutana na wadau wa vyama vya kujadili na kuondoa dosari mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na matukio360, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo Addo Shaibu amesema
hawatashiriki hadi hapo dosari zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo wa udiwani
zitakapokuwa zimeshughulikiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
“Sisi
msimamo wetu uko pale pale kwamba kuna
mapungufu makubwa sana ya kidemokrasia yanayo tokea katika michakato hii ya
uchaguzi ambayo yanapaswa kushughulikiwa ndio maana utaona tumechukua jitihada
kubwa kuwafikia wenzetu, ili kupanga
mkakati wa pamoja wa kuona jinsi ya kuyarekebisha,” amesema Shaibu.
Shaibu
amesema tangu dosari zilipotokea na kupeleka malalamiko NEC ili zishughulikiwe,
kwa mujibu wa tathmini yao inaonesha
kwamba matatizo mengi hayajashughulikiwa.
Ameongeza
kuwa baada ya vyama vya upinzani kutangaza
kususia uchaguzi NEC ilifanyia kazi suala moja tu miongoni mwa mengi
yaliyolalamikia suala hilo ni wakuu wa wilaya kuingilia uchaguzi.
Hivyo
NEC katika jambo hilo ilichukua hatua kwa kuwaandikia wakuu wa wilaya barua
ikiwataka kutojihusisha na masuala ya uchaguzi.
Amesema
hilo ni jambo dogo kwani hadi sasa hawajashughulikia suala la vyombo vya dola
kuingilia uchaguzi kwa kuvitisha na kamata kamata dhidi ya viongozi na wafuasi
wa vyama vya upinzani.
“Hilo
ni suala dogo kuna kamata kamata, matumizi ya nguvu ya kutumia vyombo vya dola
hasa polisi na jinsi na uongo katika utangazaji wa wa matokeo,” amesema.
Amesema
kuna umuhimu wa kuendelea kushinikiza ili mchakato wa uchaguzi uwe huru na
haki.
“Kwa
hiyo sasi tunaendelea kuweka shinikizo na hatutoshiriki kwenye uchaguzi huu wa
kinondoni na Siha hadi pale ambapo angalau tume itakaposhughulikia malalamiko yetu,”
ameongeza.
No comments:
Post a Comment