Alexis Sanchez kimeeleweka Man Utd...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
MCHEZAJI Alexis Sanchez(29) jana jioni amesaini mkataba wa kuichezea timu ya  Manchester United baada ya kuafikiana na klabu ya  Asernal uamisho wake wa paundi milioni 35
Mshambuliaji huyo raia wa Chile, atalipwa paund laki nne na nusu kwa wiki na mapema hii leo baada ya vipimo vya afya, atatambulishwa rasmi pamoja na muda wa mkataba wake.
Alexis Sanchez
Henrikh Mkhitaryan naye anatarajia kujiunga na Asernal mara baada ya taratibu za uamisho kukamilika ikiwa ni sehemu ya makubaliano 
Mapema jana kocha wa Manchester United Jose Mourinho alithibitisha kwamba klabu hiyo iko katika meza ya mazungumzo ya kumsajili shambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na kwamba anasubiri habari njema.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo wa Chile akajiunga na wapinzani wao katika ligi ya EPL.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search