BoT yazifunga benki tano....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imezifunga, kusitisha shughuli zote za kibenki, kufuta leseni za
kibiashara ya kibenki, benki tano na kuziweka chini ya ufilisi kuanzia leo kutokana
na kutotimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili na wakutosha.
Profesa Benno Ndulu.
Pia benki tatu kati ya nane, Kilimanjaro Coorperative Bank
Limited, Tanzania Women’s Bank Plc, na Tandahimba Community Bank Limited
zimepewa muda wa miezi sita hadi Juni 30, 2018 kuweka kiwango cha mtaji kinachokidhi
matakwa ya kisheria na kizishindwa zitafungwa.
Uamuzi huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Gavana wa BoT Profesa Benno Nduru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Banki zinazochukuliwa hatua hii Covenant Bank for Women (Tanzania) Limited,
Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers’ Coorperative
Bank Limited na Meru Community Bank Limited,” amesema Profesa Ndulu.
Amesema uamuzi huo umefikiwa kwa mujibu wa kifungu cha 56 (1)
(g), 56 (2) (a), (b) na (d), 58 (2) (i), 11 (3) (c) na (j), 61 (1) na 41 (a)cha
sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya
mwaka 2016.
Ameuhakikishia umma kuwa BoT itaendelea kulinda maslahi ya
wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.
No comments:
Post a Comment