Waziri Jafo ampa mkurugenzi Ilala siku saba...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed,Dar es Salaam


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),suleiman Jafo ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palella kuhakikisha anakarabati barabara ya Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam.


Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Suleiman Jafo (mwenye tai nyekundu) akisikiliza maelezo kutoka kwa mganga mfawidhi hospitali ya Mnyamani, Dk Isack Makundi leo jijini Dar es Salaam alipotembelea kituo hicho kuona utendaji kazi wao na changamoto




Ametoa agizo hilo leo, wakati alipotembelea barabara hiyo ili kuona changamoto na malalamiko ya barabara hiyo kwa wananchi wa eneo hilo pamoja na utupwaji taka jirani na hospitali ya Myamani.


Amesema endapo barabara hiyo haitakarabatiwa hataweza kuvumilia na kwamba atawafukuza watumishi wazembe huku akimtaka Mkurugenzi kuwasiliana na Mamlaka ya Maji safi na maji taka (DAWASCO) kudhibiti mabomba yaliyopasuka.


"Kama mkiamua kuifunga hii barabara sawa... Lakini nikipita nikakuta kazi haijaanza mtaniona mbaya.


"Watu wanapoteza maisha, nikute watu wanafanya kazi... Nawapa 'Black and white' nikikuta uzembe nitaondoka na mtu hapa,"amesema.


Akizungumzia utupaji taka jirani na hospitali ya Mnyamani, Jafo amepiga marufuku kutupa taka eneo hilo na kuagiza kufanyiwa maboresho hospitali hiyo.


 Mkurugenzi wa Ilala, Palella amesema atatekeleza agizo hilo na kwamba wapo kwenye mchakato wa kuboresha hospitali hiyo.


"Tumeshatenga fedha za fidia kwa kaya 9 sh milioni 489 ili kupisha uboreshaji wa hospitali... Leo tutakaa na Dawasco kupanga mpango kazi ili kuanza kukarabati barabara, "amesema.


Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa amesema ameshafanya ziara eneo hilo mara kumi hivyo amempongeza waziri Jafo kufika na kuchukua hatua.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search