Majimaji wajitapa....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi wetu,Songea
Timu ya Majimaji imesema kwa sasa mipango yao ya kufanya vizuri kwa mechi zijazo inaweza kutimia kutokana na kurejea kwa nyota wao wanne tegemezi waliokosekana katika mechi mbili mfululizo na hivyo kuwafanya washindwe kupata matokeo na kuambulia vichapo .
Kikosi cha timu ya soka cha Majimaji 'Wanalizombe'
Majimaji inayoendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Majimaji Songea chini ya kocha mkuu, Peter Mhina imepoteza mechi hizo ambapo mchezo wa 11 ilikutana na Ruvu Shooting na kuchapwa mabao 2-1, pia Disemba 30 mwaka jana ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Wachezaji walikosekana kwa mechi hzio ni Selemani Selembe , Paul Mahona, Tumba Sued pamoja na Abdallah Salamba ambao hawakuwepo katika kikosi hicho kutokana na matatizo mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Klabu hiyo kupitia kwa Ofisa habari wao, Onesmo Ndunguru inaeleza tayari wachezaji watatu wamesharejea na kujiunga na wachezaji wenzao kwenye mazoezi isipokuwa Abdallah Salamba bado yupo kwao.
‘’ Salamba hajarejea hadi sasa na aliondoka hapa kwa ruhusa maalumu kutokana na kupata taarifa kwamba nyumbani kwao kuna matatizo ya kifamilia ,lakini yote kwa yote anaweza akarejea hata ndani ya wiki ijayo,’’
Aliongeza "Ni imani yetu kwamba kurejea kwa wachezaji hao kutakipa kikosi nguvu ya kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho (FA) pamoja na mechi mbili zilizo mbele yetu tutakazocheza Uwanja wa nyumbani,’’alisema Ndunguru
Amesema wanaiona michezo hiyo kuwa migumu kwao kwani timu wanazokutana nazo siyo lelemama na huwa hazifungwi kizembe ,kwa hiyo wasipojipanga vyema wanaweza kuwa katika hali mbaya zaidi kutokana na pointi 11 walizonazo kwa mechi 12.
Ndunguru amesema "Tuna mechi na Azam FC Januari 18 na baada ya hapo tutawasubiri Singida United Januari 22 mwaka huu ambapo nao ukiangalia si mchezo rahisi kutokana na hawa wapinzani wetu kuwa tishio pamoja na kwamba ni wageni Ligi Kuu."
Wapinzani hao wa majimaji wapo katika nafasi nzuri kimsimamo ambapo Azam inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 26 huku Singida United ikiwa nafasi ya tatu kwa kuvuna pointi 23 kwa mechi 12 zilizocheza timu hizo .
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment