Waziri aiagiza Takukuru kukichunguza chuo cha umma Mbeya...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Mbeya
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameagiza TAKUKURU mkoani Mbeya kufanya uchunguzi wa kina katika chuo cha utumishi wa umma kama kinajihusisha na vitendo vya rushwa na kutoa ajira kwa wasiokuwa na sifa.
Mwalimu wa somo la Kompyuta, John William alimwomba waziri kufanya uchunguzi ili kubaini madudu yaliyopo katika chuo hicho hususan kuangalia sifa za waajiriwa kama wanastahili kufundisha chuoni hapo.
"Waziri msema kweli daima mpenzi wa Mungu ni vyema nikasema ukweli kuliko kukaa na kitu moyoni taarifa iliyosomwa na uongozi imeficha vitu mimi ni miongoni mwa walimu ambao nimelalamikia sana hata wizarani kuhusiana na uongozi wa chuo uliopita na wa sasa hadi nilifikia hatua ya kufukuzwa kazi kwa ajili ya kusema kweli, " alisema.
Kufuatia kauli hiyo waziri alisema wizara yake haitosita kumchukulia
hatua kiongozi yoyote ambaye kwa namna moja hama nyingine anaendesha taasisi ya serikali kwa ukilitimba na kwamba ni vyema TAKUKURU wakalifanyia kazi ili apate ukweli.
"Wizara yangu imebeba sekta nyingi ikiwemo kitengo cha rushwa sasa
watafuatilia kwa kina , na ninawaagiza kufanya kazi kwa kuzingatia
kanuni za utawala bora katika kusimamia utumishi wa umma kwa
viongozi,"alisema.
Katika hatua nyingine ameagiza wakurugenzi, makatibu tawala
mikoani kuacha ukiritimba wa kukaa na barua za watumishi maofisi
zinazotakiwa kufikishwa wizarani kwa ajili ya kuomba uhamisho kutoka
kituo kimoja kwenda kingine kwa chuki zao binafsi .
Alisema "Kama wizara wanataarifa za kuwepo kwa tabia hiyo sasa
kama mmeshindwa kuidhinisha barua za watumishi zinazowafikia ni
vyema kutoa fursa kwa watumishi waziwasilishe kwa sisi waajiri wao
kama nyinyi mmeshindwa kutekeleza majukumu yenu mliyopewa na serikali."
Katibu Tawala Mkoa, Mariam Mtunguja aliomba watumishi wa Sekta za
umma kama kuna mapungufu yanayojitokeza katika uongozi na vyema
kuwasilisha katika ngazi ya mkoa na si kufikia hatua ya kudhalilisha
mbele ya uongozi wa ngazi za juu.
Alisema "Ni jambo la aibu kwa taswira iliyojitokeza kwa viongozi wa
chuo kwa kushindwa kukaa meza moja kumaliza tofauti zenu, na kwamba suala la kutoa ajira kwa watu wasiokuwa na sifa halikubaliki hata kidogo licha ya kuagizwa TAKUKURU na kama mkoa tutafuatilia."
Kwa upande wake mkuu wa chuo, Heriel Nguvava aliomba Serikali kufanya mazungumzo na halmashauri ya jiji ili kulinunua jengo la chuo hicho kwa lengo la kupunguza gharama za kodi ambapo kwa mwezi wanalipia pango sh milioni 22
Rais wa serikali ya wanachuo, Daud Thomas aliomba wizara kuona namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa mabweni,mgahawa wa chakula kwa bei nafuu na upatikanaji wa vitabu vya kutosha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora, George Mkuchika, Akizungumza na wananchi wa kata ya Iyela Jijijini hapa alipokwenda kuzungumza na wanaufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Ametoa agizo hilo mara baada ya kuzungumza na watumishi na walimu na kumueleza malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhishwa kwa viongozi wa chuo hicho jambo linalochangia chuki, fitna, majungu katika majukumu ya kila siku.

About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment