CUF yatimiza miaka 25 ya siasa nchini...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
CHAMA cha wananchi (CUF) kimetimiza miaka 25 tangu
kipate usajili wa kudumu Januari, 21 1993 kikiwa ni chama cha kwanza katika vyama vipya vya siasa kupata usajili wa kudumu kufuatia kutimiza masharti ya usajili huo kama yalivyoainishwa kwenye Sheria namba 5 ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa.
Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa mwanzo wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipokea hati ya usajili wa kudumu kutoka kwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Marehemu Jaji Abdulwahid Borafia. Wengine kwenye picha ni Katibu Mkuu wa mwanzo wa CUF, Marehemu Shaaban Khamis Mloo, Naibu Mkurugenzi wa mwanzo wa Vijana, Mhe. Mohamed Ali Mohamed, Katibu wa mwanzo wa Makamu Mwenyekiti, Mhe. Mohammed Ali Shamte, na Mkurugenzi wa mwanzo wa Haki za Binadamu, Dr. Camillus Kassala.
CUF kiliundwa Mei 28, 1992 kikiwa ni muungano wa vikundi viwili vilivyokuwa vikipigania mageuzi, KAMAHURU kutoka Zanzibar na CIVIC MOVEMENT kutoka Tanganyika.
Sherehe za kutia saini Hati ya kuunganisha vikundi hivyo viwili zilifanyika kwa siri katika mtaa wa Kokoni, mjini Zanzibar kwenye nyumba ya marehemu Bi Toti Abdullah. Nyumba hiyo baadaye mwenyewe aliipa jina la Beit El Haq.
Baada ya hapo Juni 25, 1992 kulifanyika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa IFM, mjini Dar es Salaam kutangaza kuundwa kwa CUF.
Julai mosi, 1992 ndipo mfumo wa vyama vingi vya siasa ulipoanza kufanya kazi rasmi na CUF kupata usajili wa muda mnamo Agosti 17, 1992.

No comments:
Post a Comment