Makonda awasaka matapeli Dar es salaam...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo waliodhulumiwa mali zao ikiwemo viwanja, nyumba, shamba, gari na vitu tofauti  kufika ofisi ya mkuu wa mkoa Ilala Boma kuanzia Januari 29 hadi Februari 02, 2018 ili kupatiwa  msaada wa kisheria.

Paul Makonda

Taarifa yake kwa umma inaeleza kuwa Makonda ameandaa magwiji wa sheria wa kutosha kwa lengo  la kuwasikiliza.

"Cha muhimu ni kufika na nyaraka na vielelezo halali  ili mpatiwe haki zenu." Inaeleza taarifa hiyo

"Hii ni baada ya RC Makonda kubaini uwepo wa baadhi ya wananchi wanyonge wanaodhulumiwa na kunyanyasika kwa kuporwa haki zao na watu wenye uwezo kifedha au wanasheria wenye utaalamu unaokandamiza wanyonge."

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search