Donald Trump, Kim Jon-un watunishiana misuli....soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
Rais wa Marekani, Donald Trump amejigamba kuwa kibonyezo chake cha silaha za nyuklia ni kikubwa na kilicho na nguvu zaidi kuliko kile cha kiongozi wa Korea Kaskazini,Kim Jon-un.
Rais wa Marekani, Donald Trump amejigamba kuwa kibonyezo chake cha silaha za nyuklia ni kikubwa na kilicho na nguvu zaidi kuliko kile cha kiongozi wa Korea Kaskazini,Kim Jon-un.
Rais wa Marekani, Donald Trump
Trump amejibu mapigo hayo kupitia akaunti yake ya Twitter ikiwa ni majibizano kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili yaliyo na silaha za nyuklia.
Mapema wiki hii katika salam zake za mwaka mpya 2018,Kim alionya kuwa kibonyezo chake cha nyuklia kipo kwenye meza yake.
Korea Kaskazini inadai kuwa ina silaha za nyuklia na inaweza kuishambulia Marekani huku wadadisi wakisema kuwa ikiwa Korea Kaskazini ina silaha za nyuklia, je ina teknolojia ya kuzitumia?.
Kando na kuitishia Marekani, ujumbe wa mwaka mpya wa Kim pia uliwashangaza wengi wakati alisema kuwa alikuwa tayari kwa mazungumzo na Korea Kusini na angependa kuituma timu kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini mwezi ujao.
Tayari mapema hii leo mawasiliano ya simu baina ya Korea Kusini na Kaskazini yamerejea. Tangu mwaka 2016 Korea Kaskazini ilikata uhusiano huo
Tayari mapema hii leo mawasiliano ya simu baina ya Korea Kusini na Kaskazini yamerejea. Tangu mwaka 2016 Korea Kaskazini ilikata uhusiano huo
No comments:
Post a Comment