Mbeya walilia barabara...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu, Mbeya


WANANCHI wa kata ya Mwakibete jijini Mbeya  wameiomba serikali mkoani humo kuboresha miundombinu na kujenga kwa kiwango cha lami, barabara kutoka  mtaa mwambene hadi  relini.


Diwani Kata ya Mwakibete, Agnes Mwangasila akizungumza na   wananchi katika mtaa wa Mwambene jijini Mbeya

Wakizungumza na matukio360 wamesema ubovu wa barabara hiyo ni changamoto kubwa inayokwamisha shughuli zao za kiuchumi.

"Tunaomba Serikali ya mkoa ilione hili kwani  tunashindwa hata
kushirika katika sehemu ya mazishi tunahofia vyombo vyetu vya usafiri kuharibika," amesema Thimos Mwaisenye


Diwani viti maalum kata ya Mwakibete, Agnes Mangasila (CCM)  amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo na ameiomba serikali ya mkoa hu o kuondoa kero.


Akizungumza  amesema  uchakavu wa barabara hiyo imekuwa ni changamoto kubwa jambo linalosababisha wananchi kulalamika kwa
viongozi hasa  katika kipindi cha masika.

"Tunaomba mkuu wa mkoa  atusaidie barabara  ijengwe kwa kiwango cha rami kwani ninahojiwa sana na wapigakura wangu nakosa majibu sahihi kwa kweli imekuwa ni chakavu sana ina mashimo, maji
yanatuhama na kusababisha mazalia ya mbu,"amesema diwani huyo.


Alipoulizwa kuhusu tatizo hilo, mkuu wa mkoa  huo, Amos Makalla amesema tayari ameagiza uongozi wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) kutatua tatizo hilo.


Mratibu wa  TARURA mkoa, Mhandisi Danstan Kishaka  amesema  wamepokea maagizo ya mkuu wa mkoa na tayari wameingiza kwenye mradi na kwamba ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami utafanyika.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search