Facebook kudhibiti habari za kizushi ...soma habari kamili na matukio 360...#share

Na mashirika ya kimataifa

KAMPUNI ya facebook imetangaza kuwa imebadili kampuni inayoipa habari, ili kukabiliana na kile ilichotaja kama habari za uzushi na za kupotosha.
Mark Zuckerberg

 Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ya facebook, Mark Zuckerberg, amesema mtandao wake sasa utakuwa ukiwauliza watumiaji wake ni vyanzo vipi vya habari wanaamini zaidi na hivyo kuwapa nafasi ya kwanza.

Waandishi wa habari wanasema kuwa kampuni hiyo ya facebook ambayo ina zaidi ya watumiaji bilioni mbili, inataka kusitisha usambazaji wa habari bandia na propaganda, baada ya mahusiano yaliyotajwa na malumbano na mashirika ambayo yana misimamo mikali ya kisiasa.



 Mapema mwezi huu, Mark Zuckerberg, alitangaza mabadiliko ya vyanzo vya habari ya kampuni hiyo, iliyonuia kuhimiza ujumbe zinazotumwa na familia na marafiki badala ya mashirika ya kibiashara na bidhaa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search