IGP Sirro akagua miradi ya Polisi...soma habari kamili na matukio360...#share


Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa  Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya  Jeshi hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi karibuni.

Wananchi wa Kigogo Mburahati jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, wakati alipofanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Jeshi hilo Mbweni jijini Dar es salaam katika wilaya ya kipolisi ya Kawe.
Picha na Jeshi la Polisi.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search