Mafuriko yauwa watu 37 ...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
Watu zaidi ya 37 wamefariki baada ya mafuriko kuukumba mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa kufuatia mvua kubwa, maafisa wa serikali wamesema.
Managing ya nyumba baada ya mvua kubwa kunyesha kutoka mji wa Kinshasa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo(DRC)
Wengi wa waliouawa ni wakazi wa mitaa ya mabanda ambapo nyumba nyingi zimeharibiwa na maji ya mafuriko na maporomo ya ardhi.
Wengi kati ya wakazi milioni kumi wa mji wa Kinshasa huishi katika makazi duni katika maeneo tambarare na miundo mbinu ya kuondoa maji taka ni duni.
Waziri wa jimbo anayeangazia masuala ya kiafya na kijamii Dominique Weloli, alisema wengi wa waliofariki ambao ni pamoja na "watoto wawili au watatu waliokufa maji" walikuwa wanaishi Ngaliema, mtaa duni ambao umeathirika sana.
"Kumetokea si tu mafuriko bali pia maporomoko ya ardhi na nyumba kadha zimebomoka," Weloli amesema.
Kumekuwa na matukio ya vifo vinavyotokana na mafuriko karibu kila mwaka msimu wa mvua kubwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search